Monday, June 29, 2015

APIGWA RISASI TATU AKIJARIBU KUTOROKA GEREZA LENYE ULINZI MKALI

Mfungwa aliyetoroka New York akamatwa

Polisi nchini Marekani wamempiga risasi na kumkamata mfungwa aliyetoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa amefungwa kutumikia adhabu kutokana na makosa ya mauaji wiki tatu zilizopita.
David Sweat alikamatwa karibu na mpaka wa Canada baada ya afisa wa polisi akiwa katika mazoezi ya kukimbia kando ya barabara.
Mfungwa mwenzake aliyetoroka Richard Matt aliuawa na polisi Ijumaa. Watu hao wawili walitumia zana imara kuweza kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali la Clinton na kusababisha msako mkubwa wa polisi kufanyika.
Gavana wa jimbo la New York, Andrew Cuomo, amesema jinamizi la wahalifu hao limekwisha.
Kwa habari, taarifa na matukio pamoja na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment