Monday, June 22, 2015

WALAJI NYAMA YA MBWA CHINA, WAPATA KIGINGI

Rekodi mpya ya ulaji wa nyama ya mbwa China!

doog
China imeingia tena kwenye headlines baada ya ulaji wa nyama ya mbwa kuongezeka nchini humo. Hapo awali ulaji wa nyama hiyo ulikatazwa nchini China baada ya kuonekana kua ulaji wa nyama hiyo ni kinyume na utaratibu wa kibinadamu kwa sababu mbwa walionekana kua viumbe venye thamani kubwa kwenye maisha ya bindamu, kwenye ulinzi na hata uwindaji pia.
Hali iko tofauti kwa karne hii ya 21 nchini China kwani ulaji wa nyama ya mbwa umeongezeka licha ya kitendo hicho kukatazwa kwa zaidi ya miaka hamsini iliopita. Kuongezeka kwa vitendo hivi kumesababisha mjadala mkubwa nchini humo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu ambao wanapinga kitendo hicho huku wakidai ulaji wa nyama ya hiyo ni ukatili dhidi ya wanyama hao, na ni kitendo kinacho dumisha dhana potofu za ulaji wa nyama ya mbwa.
chiinaa
Kutokana na historia ya China, Guangzhou ni mji unaofahamika kwa watu wanao ongoza kwa ulaji wa nyama ya mbwa, lakini hivi karibuni mgahawa maarufu wa nyama ya mbwa ulilazimika kufunga biashara baada ya miaka 51 ya utengenezaji wa nyama hiyo jijini hapo baada ya vita dhidi ya watetezi wa haki za wanyama wa kufugwa (Domestic Pets). Licha ya hivyo, uchinchaji wa mbwa kwa ajili ya uuzaji wa nyama ulikua maarfu sana jijini Beijing lakini kitendo hichi kilifika mwisho miaka 10 iliopita kutokana na Sheria mpya iliokataza kitendo hicho.
Bado kuna miji ambayo vitendo vya ulaji wa nyama ya mbwa vinaendelea kwa kiasi kikubwa, ila maandamano ya kukomesha tabia hii yameshaanza kwa baadhi ya miji nchini humo, wakiwa na dhamira ya kukomesha kitendo hicho.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment