Monday, June 22, 2015

TAARIFA KUTOKA SOUTH AFRIKA

South Africa kwenye headlines na vurugu alizofanyiwa Rais Jacob Zuma bungeni!!

jacob-zuma-1
Tarehe 19 June mwaka huu Bunge la South Africa liliingia kwenye headlines katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii baada ya baadhi ya viongozi kutoka chama cha upinzani kuanzisha vurugu zilizo pelekea kuahirishwa kwa Bunge hilo siku ya ijumaa.
Bunge la South Africa liliingia vurugu baada ya wanachama wa Economic Freedom Fighters kumzuia Rais Jacob Zuma kuendelea kutoa ripoti aliokusudia kuwasilisha mbele ya Bunge hilo kwa kumshambulia Rais huyo na maswali yanayohsu uwajibikaji wake, maswali ambayo yaliongaishwa na malalamiko ya yeye kukiuka Katiba ya nchi hiyo, kitendo kilichopelekea Rais huyo kutokupewa nafasi ya kujieleza.
Kitendo hichi kilimlazimu Spika wa bunge Baleka Mbete kuahirisha Bunge hilo na kuita kikao cha dharula na vyama hivyo nje ya Bunge hilo baada ya vurugu kutapakaa Bungeni hapo, na alipohojiwa na vyombo vya habari, Spika wa Bunge la South Africa alisema amesikitishwa na kitendo hiki kufanyika na baadhi ya watu wanaotazamwa na jamii kama viongozi, na kuongeza kua, kitendo hicho sio mara ya kwanza kutokea… iliwahi kutokea mwezi Agosti tarehe 21 mwaka jana ambako pia alilazimika kuahirisha Bunge hilo kutokana na vurugu kuanzishwa na vyama vya upinzani.
Bunge la South Africa limepinga baadhi ya malalamiko kutoka kwa viongozi wa vyama vya upinzani kua Rais Jacob Zuma anakiuka Katiba na kuepuka uwajibikaji na kusema kua Rais huyo anategema kuonekana tena Bungeni mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya kutoa ripoti hio kama Sheria ya nchi inavyomtaka kufanya hivyo mara nne kwa mwaka na mara moja kwa mwaka katika Baraza la taifa la majimbo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment