Bondia kufariki baada ya pambano kumalizika..
         
Bondia Davey Browne ambaye ni raia 
wa Australia amepoteza maisha siku nne baada ya kupoteza fahamu kufuatia
 kipigo cha ‘knock out’ katika pambano la ngumi huko Sidney.
Mwanamasumbwi huyo mwenye miaka 28 
alidondoka chini baada ya kupigwa na mpinzani wake Carlo Magali wa 
Ufilipino katika raundi ya 12 katika uzani wa super-featherweight ijumaa
 iliyopita.
Baada ya kupoteza fahamu alipelekwa hospitali katika chumba cha wagonjwa mahututi hadi mauti ilipomkuta.
Kwa habari, matokeo na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog 
No comments:
Post a Comment