Pale ambapo ubunifu unasababisha ajikute Mikononi Polisi, saa ikafananishwa na Bomu…
         
Ahmed Mohamed
 ni kijana wa miaka 14, alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kufanya 
ubunifu ambao yeye alidhani itakuwa ni kitu kizuri kuwafurahisha Walimu 
wake, lakini baada ya kuwaonesha tu ubunifu wake, ikapigwa simu Kituo 
cha Polisi na wakamkamata !!
Ahmed ni mwanafunzi wa MacArthur High School
 iliyoko Irving, Texas Marekani… ni kijana ambae ana kipaji cha kufanya 
ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali nyumbani kwao, alienda Shule na 
kisanduku kidogo ambacho alikifanyia ubunifu na kubadilisha kisanduku 
hicho kuwa saa.
Walimu walipomkuta na kifaa hicho 
walitoa taarifa Polisi, wakamkatamata ili akatolee maelezo vizuri kuhusu
 hiyo saa yake… kilichowashtua Walimu ni nyaya nyaya nyingi kwenye huo 
ubunifu wa saa, Polisi wanasema huenda huyo mtoto akafunguliwa mashtaka 
ya kutengeneza bomu feki kwa lengo la kutisha watu !!
Ahmed
 amesema Polisi wamemhoji kwa nini ametengeneza Bomu? lakini 
amewasititizia mara zote kwamba kile kifaa sio Bomu ila ni saa ambayo 
aliibuni mwenyewe.
Polisi walimwachia huku uchunguzi 
ukiendelea lakini baba yake anaonekana kukasilishwa sana huku akihisi 
kwamba kuna ishu ya ubaguzi wa Kidini kwenye suala la mtoto wake 
kukamatwa kwa tuhuma hizo.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:
Post a Comment