Je,ulaji wa zaidi ya ndizi 6 kwa mpigo unauwa?
Mara nyingine husemekana kwamba ulaji wa ndizi nyingi kupita kiasi kwa mpigo unaweza kuhatarisha maisha yako.
Imedaiwa zaidi kwamba ulaji wa zaidi ya ndizi sita kwa mpigo unaweza kukuuwa.Je, hili ni kweli?Ndizi ni mojawapo ya matunda yenye umaarufu mkubwa duniani yenye vitamini na madini.
Kwa upande huo ndizi huonekana kuwa na manufaa makubwa kwa mwili wa binaadamu,kwa hivyo basi kwa nini watu huwa na fikra kwamba matunda hayo yanaweza kuwa hatari na hata kuuwa?
Mmoja ya watu maarufu ambao wamekuwa wakisambaza ujumbe huo ni Karl Pilkinton rafikiye msanii mcheshi Ricky Gervais.
Madini ya Potasiam yaliomo katika ndizi ni ya viwango vya juu na ni hatari iwapo tayari umekula ndizi sita.
Je, madini ya potosium yana hatari gani? Kwa kweli ni muhimu katika maisha ya mwanadamu na hupatikana katika seli zote za mwili wa mwanadamu kulingana na mtaalamu wa chakula Catherine Collins kutoka hospitali ya St George's mjini London.
No comments:
Post a Comment