COASTAL UNION YALOWA JANGWANI
MABINGWA
watetezi, Yanga SC wameanza vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal
Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaipeleka Yanga SC kileleni mwa LIgi Kuu baada ya mechi nane za mzunguko wa kwanza, ikiongoza kwa wastani wa mabao.
Mchezaji bora na mfungaji bora wa LigiKuu msimu uliopita, Simon Happygod Msuva ndiye aliyefunga bao la kwanza la Yanga SC msimu huu, dakika ya saba akimalizia pasi ya Amisi Tambwe.
Lilikuwa bao ambalo lilitokana na kazi nzuri ya yeye mwenyewe Msuva, aliyepokea pasi ya Haruna Niyonzima nje ya boksi na kuingia nayo ndani kabla ya kumpasia Tambwe aliyemrudishia mfungaji haraka kwa mbele kidogo.
Kocha Mganda, Jackson Mayanja alifanya mabadiliko mapema tu baada ya bao hilo akimtoa mchezaji wa zamani wa Simba SC, Adeyoum Saleh Ahmed na kumuingiza mchezaji mwingine wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Twaha Ibrahim ‘Messi’.
Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 42 na ushei akimalzia mpira uliodondoka baada ya kugongwa kwa kichwa na beki wa Coastal, Tumba Lui Swedi aliyeruka na Mrundi Amisi Tambwe kugombea krosi ya Simon Msuva.
Kipindi cha pili, Coastal Union walibadilika na kucheza vizuri, lakini wakaishia kupoteza nafasi nzuri mbili kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa SImba SC, Ally Ahmed ‘Shiboli’.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela dk90, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk69, Donald Ngoma na Godfrey Mwashiuya/Deus Kaseke dk73.
Coastal Union; Sabwato Nicholas Godfrey Wambura/Mbwana Hamisi ‘Kibacha’ dk62, Hamad Juma, Yassin Mustafa, Ernest Joseph Mwalupani, Tumba Swedi, Said Jeilan/Patrick Protas dk52, Ali Ahmad, Youssoufa Sabo, Nassor Kapama na Adeyoum Saleh Ahmed/Twaha Ibrahim ‘Messi’ dk22.

Simon Msuva (kushoto) akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza |
Beki wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali (kushoto) akiwatoka wachezaji wa Coastal Union |
Beki wa Coastal, Tumba Lui Swedi akiondosha mpira miguuni mwa winga wa Yanga SC, Godfrey Mwashiuya |
Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma akiwania mpira dhidi ya beki wa Coastal, Yassin Mustafa |
Lilikuwa bao ambalo lilitokana na kazi nzuri ya yeye mwenyewe Msuva, aliyepokea pasi ya Haruna Niyonzima nje ya boksi na kuingia nayo ndani kabla ya kumpasia Tambwe aliyemrudishia mfungaji haraka kwa mbele kidogo.
Kocha Mganda, Jackson Mayanja alifanya mabadiliko mapema tu baada ya bao hilo akimtoa mchezaji wa zamani wa Simba SC, Adeyoum Saleh Ahmed na kumuingiza mchezaji mwingine wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Twaha Ibrahim ‘Messi’.
Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 42 na ushei akimalzia mpira uliodondoka baada ya kugongwa kwa kichwa na beki wa Coastal, Tumba Lui Swedi aliyeruka na Mrundi Amisi Tambwe kugombea krosi ya Simon Msuva.
Kipindi cha pili, Coastal Union walibadilika na kucheza vizuri, lakini wakaishia kupoteza nafasi nzuri mbili kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa SImba SC, Ally Ahmed ‘Shiboli’.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela dk90, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk69, Donald Ngoma na Godfrey Mwashiuya/Deus Kaseke dk73.
Coastal Union; Sabwato Nicholas Godfrey Wambura/Mbwana Hamisi ‘Kibacha’ dk62, Hamad Juma, Yassin Mustafa, Ernest Joseph Mwalupani, Tumba Swedi, Said Jeilan/Patrick Protas dk52, Ali Ahmad, Youssoufa Sabo, Nassor Kapama na Adeyoum Saleh Ahmed/Twaha Ibrahim ‘Messi’ dk22.
No comments:
Post a Comment