Majibu ya Mourinho kuhusu mfululizo wa matokeo mabovu na kuelekea mechi dhidi ya klabu ya Maccabi Tel Aviv..
Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho
ambaye ni mtaalam wa kucheza na saikolojia za makocha na wachezaji wa
timu pinzani ili aweze kushinda, kwa sasa yupo katika wakati mgumu na
klabu yake ya Chelsea kwani bado haijafanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu.
Licha ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza msimu uliyopita, klabu ya Chelsea chini ya kocha Jose Mourinho imecheza mechi 5 za Ligi Kuu Uingereza na kushinda moja, sare moja na kupoteza mechi tatu. Hivyo September 15 katika Press Conference na waandishi wa habari, Jose Mourinho ameongea kuhusu hali ilivyo katika vyumba vya kubadilishia nguo.
” Hili ni
swali ambalo limeendelea kuulizwa mara kwa mara lakini jibu ambalo
utataraji ni lile lile, hali za wachezaji katika vyumba vya kubadilishia
nguo ni kuwa kuna wakati wa kutabasamu na kutaniana nafikiri hilo ni
jibu la msingi. Kama watu hawapati mafanikio unatakiwa mpambane ili
mfanikiwe nakuahidi tunafanya kazi kwa bidii”>>> Mourinho
“Tatizo
pekee tulionalo ni mfululizo wa kutopata matokeo mazuri tunajua na
hatufurahishwi na hii hali, ila unaweza kuniuliza kwa nini makocha
wengine hawapo katika wakati mgumu licha ya kutofanya vizuri kwa miaka
mitano, saba au kumi? lakini mimi bado ni bingwa wa Ligi Kuu Uingereza
kwa nni nipate wakati mgumu”>>> Mourinho
Hayo ni baadhi ya majibu ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho
ambaye amejibu kuhusu yeye kuwa na wakati mgumu kwa sasa, hizo ni kauli
zilizotoka wakiwa wanaelekea kucheza mechi yao ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Maccabi Tel Aviv September 16.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchanlog
No comments:
Post a Comment