Tangakumekuchablog
Tanga, MJUMBE
wa Baraza kuu la Vijana Taifa,, Deo Ndejemba, amewataka vijana kujitokeza kwa
wingi siku ya upigaji kura kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa
kimbunga.
Akizungumza katika kikao cha Umoja
wa Vijana wa CCM kutoka makundi mbalimbali ya kiwemo ya Vyuo Vikuu na Shule za
Sekondari leo, Ndenjemba alisema ushindi wa CCM uko mikononi mwa vijana.
Aliwataka kufanya mikutano mfululizo
hadi muda wa mwisho wa kampeni ili kila kijana mmoja anavuna vijana watano
ambao siku ya kupiga kujihakikishia ushindi wa kimbunga.
“Kwa hamasa ilivyo kila niendako ni
wazi kabisa kuwa mwaka huu chama cha mapinduzi kitapata ushindi wa
kimbunga----hapa Tanga dalili zinaonyesha Nundu ameshinda” alisema Ndejemba
Aliwataka vijana hao kipindi hiki
cha kampeni za uchaguzi Mkuu kuwa
watulivu na kuvumiliana katika mambo mbalimbali ya kisiasa ili Taifa limalize
uchaguzi kwa amani na utulivu kama uliopo.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo
la Tanga mjini, Omari Nundu, alisema akichaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha
hakuna kijana anaelalamika kukosa kazi na kudai kuwa ziko nyingi ila nyenzo
hawana.
Alisema vijana wengi wamekuwa
wakilalamika kukosa kazi jambo ambalo Mbunge huyo amepinga na kusema kuwa kazi
ziko nyingi ila tatizo hawana vyenzo za kufanyia kazi.
“Kazi ni nyingi na naweza kusema
kuwa nyenzo ndio hakuna laini niwaombe nikichaguliwa tena vipaumbele vyangu ni
vijana kufanya kazi----sitokuwa tayari kuona kijana analalamika hana kazi”
alisema Nundu
Alisema ili kuweza kuyafanya hayo
amewataka wananchi wa jimbo la Tanga mjini kumchagua yeye kwa madai kuwa yuko
na uwezo wa kuyafanya kwa kushirikiana
na Serikali pamoja na wananchi.
Mjumbe wa Baraza kuu la Vijana Taifa
(CCM), Deo Ndejemba, akisalimianma na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya
Tanga mara baada ya kuwasiliki kushiriki katika kikao cha Jumuiya ya Vijana
kujadili mikakati ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu October 25.
Wanachama na washabiki wa CCM Tanga, wakifurahia jambo wakati wa kikao cha Jumuiya ya Vijana CCM Wilaya ya Tanga wakati wa kikao cha mikakati ya ushindi kuelekea Uchaguzi mkuu October 25.
No comments:
Post a Comment