Tangakumekuchablog
Lushoto,
MWENYEKITI wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amewaongoza maelfu ya wakazi wa
jimbo la Lushoto katika mazishi ya aliekuwa mgombea wa Chama hicho,Mohammed
Mtoi aliekufa kwa ajali juzi na kuzikwa jijini kwano Mkuzi.
Viongozi waliohudhuria mazishi hayo
ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Maryam Jumaa, John Mnyika, Mwesiga
Beregu, Halima Mdee, Naibu katika mkuu Zanziba Salumu Mwalimu, Mgombea Ubunge
jimbo la Ilala, Hassan Hassanal na wengine wengi kutoka vyama vya vinavyounda
Ukawa.
Akitoa salamu zake , Mbowe alisema
Mtoi alikuwa kijana ambaye amechomoza katika siasa na kuungwa mkono na watu
wengi na kuonyesha kuwa kipenzi cha walio wengi.
Alisema jimbo la Lushoto litampata
mbadala wa Mtoi ila kwa wakati huu Chadema na familia ya Mtoi inaomboleza kifo
cha kijana huyo ambaye amewacha pengo kubwa ndfani ya chama.
“Chadema na familia ya Mtoi
inaomboleza kwa kuondokewa kwa kijana ambaye nyota yake ilikuwa inachomoza kwa
kasi----kwa sasa jimbo halitakuwa na mgombea Ubunge “ alisema Mboe
Kwa upande wake, John Mnyika alisema
yeye ni rafiki mkubwa wa Mtoi na ndie aliemshawishi kuingia katika Chama na
kuwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Lushoto.
Alisema alimshawishi kutoka katika
ualimu na mara baada ya kuingia katika siasa alikuwa na nyota inayong’ara na
dalili za kuwa Mbunge zilikuwa zinachomoza.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji wa CUF Wilaya ya Lushoto, Gogola Shechonge, alisema Chama chake
kitaendeleza kumsimamisha mgombea wake jimbo la Lushoto .
Alisema uongoza wa Chama Taifa
alitoa uamuzi wa Chadema kugombea jimbo la Bumbuli lakini hawakufanya hivyo na
kung’ang’ania jimbo la Lushoto ikiwa ni tofauti ya makubaliano.
Alisema CUF itaendelea kukiachia
Chadema jimbo la Bumbuli na kuwaunga mkono na hivyo kukitaka kufuata
makubaliano ya uongozi wa juu Taifa ili kuendeleza mshikamano wa Umoja wa
Ukawa.
Mwiho
Maelfu ya wakazi wa Lushoto na wafuasi wa Chadema wakiwa wamefurika nyumbani kwa aliekuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Lushoto kupitia Chadema jana
Viongozi mbalimbali wa Chadema Taifa wakiwa katika maomboleza ya kifo cha aliekuwa mgombea wa Chadema jimbo la Lushoto, Mohammed Mtoi jana kijijini kwao Mkuzi.
Wafuasi na washabikiwa Chadema, jimbo la Lushoto wakiswalio sala ya Jeneza ya aliekuwa mgombea Ubunge jimbo la Lushoto Mohammed Mtoi na kuzikwa jana kijijini kwao, Mkuzi.
No comments:
Post a Comment