Mwanamke kapigwa faini na Askari, lakini bado akaongeza na ‘ASANTE’ yake juu…
Ni kawaida sana kutokea mtu amekosea
kabisa barabarani akiwa anaendesha gari lake, trafiki akamkamata kwa
kufanya kosa lakini bado mtu huyohuyo atalalamika kweli, kama ameonewa
hivi !!
Umewahi kusema neno ‘ASANTE’ kwa mtu
aliyekuadhibu kwa vile umefanya kosa? Mama wa Kimarekani amefanya hivyo
kirahisi kabisa baada ya kukamatwa na Officer wa Police ndani ya
Georgia, Marekani.
Mama huyo alikamatwa na Police kwa kosa
la kuzidisha speed, akapigwa faini… lakini kwa kuonesha kwamba
analitambua kosa lake, aliamua kuandika na barua kabisa kumshukuru
Askari huyo kwa kumkamata kwa kosa hilo na kumpiga faini pia.
‘Bwana
Officer, ni aibu yangu kwa kosa la kuzidisha spidi. Yako mengi mabaya
yanazungumzwa na watu kuhusu Maafisa wa Polisi na kazi yenu ni hatari
sana. Naomba utambue kwamba mimi pamoja na Familia yangu tunajiona wenye
bahati kulindwa na watu wazuri kama nyie, ASANTENI SANA‘
Hii ndio picha ya Barua hiyo ambayo mwanamke huyo aliiandika kwa Polisi..
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment