Monday, September 7, 2015

WACHEZAJI WA AFRIKA WATAJWA KUENDEKEZA UGANGA (JUJU)

Imani za kishirikina katika soka zaingia katika headlines Uingereza….

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kuwa katika mchezo wa soka hususani katika bara la Afrika, kuna baadhi ya viongozi na wachezaji wanaamini kupata mafanikio katika soka kwa ushirikina. Kwa mujibu wa mtandao wa mirror.co.uk umetaja kuwa wachezaji waliyo wengi wa Afrika wanaocheza Ligi Kuu Uingereza ushiriki katika imani hiyo.
Mtandao huo umemtaja Emmanuel Adebayor kuamini katika imani hiyo, kwani Adebayor ambaye amewahi kukaririwa na vyombo vya habari akimtuhumu mama yake na dada yake wanamroga ili asifanikiwe katika soka.
West-Brom-v-Stoke-City
Brown Ideye
Wachezaji wa Afrika wanatajwa kulipa pesa nyingi kwa waganga (JUJU MEN) na kupewa masharti ya namna ya kufanya ili wafanikiwe mambo yao, tabia hii inadaiwa kufanyika katika nchi za Afrika Magharibi ambapo wachezaji hupewa uganga ili wasipate majeruhi na kupunguza majeruhi.
Brown Ideye kutokea Nigeria ambaye amewahi kuichezea West Bromwich Albion ya Uingereza amewashauri wanaopenda njia ya mkato katika soka.
“Nawajua wachezaji wanaojihusisha na imani za kishirikina hawawezi kutoka katika huo mfumo, wameweza kupata mafanikio kwa haraka lakini inawagharimu kwa muda mrefu, ushirikina una ushawishi mkubwa, waganga wanaokwambia kuwa wataweka maisha yako sawa ni njia zao za kujitajirisha”>>> Brown Ideye
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment