Utatamani kuyaona mazuri ya Nigeria 2016? Na huu mjengo kama wa Marekani utakuwepo !!
Kwenye list ya nchi ambazo zina uchumi
mzuri zaidi Africa, Nigeria imo… YES, yani hata ukizitaja tatu bora nayo
imo… Nigeria imetajwa kama nchi yenye uchumi mzuri mwaka 2015 na
yenyewe inashika nafasi ya tatu, wakati ya kwanza ni South Africa na ya
pili ni Egypt !!
Lakini kama unakumbuka vizuri, September
11 kila mwaka nchi ya Marekani ina kumbukumbu ya tukio la shambulio la
Kigaidi lililotokea New York, kwenye Jengo kubwa la Biashara la Kimataifa, World Trade Center mwaka 2001.
Sasa jina la World Trade Center linakuja Africa,
Mjengo unashushwa rasmi kabisa katikati ya Jiji la Abuja Nigeria… kitu
kitakuwa ni cha kisasa na ndani yake kutakuwa na vyumba vya Biashara
pamoja na apartments ambazo watapangishwa watu na watakuwa wanaishi kama
home tu yani !!
Unaambiwa mpaka hiki kitu kikikamilika
kitakuwa kimeweka Rekodi ya kuwa Jengo kubwa zaidi Afrika Magharibi
ambalo ndani yake kuna shughuli za aina nyingi zinafanyika.
Ufunguzi wa Jengo hilo utafanyika mwaka 2016 ambapo awamu ya kwanza ya Ujenzi itakuwa imekamilika.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment