Mtoto aliyekamatwa na saa wakidhani ni bomu harudi tena Shule? Boss wa Facebook nae kaandika haya..
Stori bado inagusa kwenye vichwa vya habari Duniani, September 16 nilikusogezea stori ya Ahmed Mohamed mtoto
mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikamatwa Shuleni na kupelekwa Polisi
baada ya kukutwa na saa aliyoibuni yeye mwenyewe lakini Walimu na Polisi
walidhani ni Bomu !!
Siku iliyofuatia Rais wa Marekani, Barack Obama aliguswa, akaandika kwenye ukurasa wake Facebook kwamba anamkaribisha ndani ya Ikulu ya Marekani kama njia ya kufanya watoto wapende somo la Sayansi.
Ahmed alikuwa mwanafunzi wa Shule ya MacArthur High School iliyoko Irving, Texas Marekani… kingine kuhusu yeye leo ni kwamba Baba wa Ahmed, Mohamed Elhassan Mohamed amethibitisha kwamba Familia haiko tayari kumrudisha Ahmed Shuleni hapo.
Japo Polisi waliridhika na Uchunguzi
kwamba kifaa alichokamatwa nacho sio Bomu, msimamo wa Shule uko
palepale… wanasema hairuhusiwi mwanafunzi kuja na vitu ambavyo
vimekatazwa Shuleni hapo, kwa hiyo hata hiyo ya Ahmed kukamatwa hawako tayari kuomba radhi.
Boss mwenyewe wa Facebook, Mark Zuckerberg amempongeza Ahmed
kwa kipaji chake huku akisema kwamba mtoto huyo alitakiwa kupongezwa na
sio kukamatwa na Polisi, kwa sababu Dunia inawahitaji zaidi watu kama
yeye.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment