Unamkumbuka Rivaldo wa FC Barcelona? Kafanyiwa upasuaji taarifa ipo hapa…
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Brazil Rivaldo bado dunia ya soka ina mkumbuka kwa umahiri wake uwanjani lakini amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’or mwaka 1999. Mwaka 2004 aliingia katika list ya wachezaji bora 100 wa FIFA waliohai.
Rivaldo ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil waliotwaa Kombe la Dunia 2002, kwa sasa ni Rais wa klabu ya Mogi Mirim na
amepost picha katika mtandao wa kijamii inayoonyesha amefanyiwa
upasuaji wa goti lake la kulia, hivyo hiyo ni ishara ya kuwa upasuaji
huo umefanyika kwa mafanikio.
Hata hivyo licha ya Rivado kustaafu soka bado yupo mbadala wake yaani mwanaye Rivadinho amefuata nyayo za baba yake na anacheza soka, kuna wakati waliwahi kuingia katika headlines ya kucheza pamoja katika klabu ya Mogi Mirim na wote kufunga magoli. Rivaldo kwa sasa ana umri wa miaka 43.
Hii ni video ya Rivaldo na Rivaldinho wakifunga magoli katika mechi moja
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment