Tangakumekuchablog
Tanga, MKUU wa
Mkoa wa Tanga aliehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalula, amemtisha zigo la
migogoro ya ardhi aliyodai kufanya na watendaji wa Idara ya Mipango miji mbadala wake , Mwantumu Mahiza aliehamia
Tanga.
Akimkaribisha Leo ukumbi
wa ofisi ya mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa, Magalula alisema migogoro ya ardhi
inasababishwa na watendaji wa mipango miji na sio wananchi hivyo kumuachia zigo
hilo ambalo limekuwa likiwatesa wananchi.
Alisema Idara hiyo imekuwa
ikiwagombanisha wananchi wenyewe kwa wenyewe pasina sababu na linapobumbuluka hutoa
visingizio vya sheria na mwaka hivyo kumtaka kulivalia njuga ikiwa na pamoja na
kulikomesha.
“Mheshimiwa dada yangu Mwantumu
Mahiza karibu Tanga na niwaage watu wa Tanga kwa kusema kwaherini-----ila kuna
jambo moja ambalo niseme waziwazi pasina kuoneana haya kuwa Idara ya mipango
miji ni mabingwa wa kugombanisha wananchi” alisema Magalula na kuongeza
“Wao ndio wanaofanya hiyana kwa
kufanya mavirigisa na ujanja ujanja halafu husikilizia----pale linapobumbuluka
hukaa pembeni kisha kutoa vifungu vya sheria na mwaka baada ya watu kugombana
kuhamasiana” alisema
Alimtaka Mkuu huyo mpya kulikomesha
tatizo hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likirudisha nyuma maendeleo ya
wananchi badala ya kufanya kazi za maendeleo wamekuwa wakipanga foleni ofisi za
mipango miji ambako ndiko kiini cha tatizo.
Akizungumza baada ya makabidhiano,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, alisema hatomuonea huruma kiongozi
yoyote katika kazi bila kujali cheo wala nasaba hivyo kuwataka kuwatumikia
wananchi kwa haki na uwazi.
Alisema yote ambayo ameelezwa na
mtangulizi wake atayafanyia kazi na yule ambaye amefanya madudu ajisafishe
kabla ya operesheni katika ofisi na idara hajaianza.
“Mheshimiwa Magalula changamoto na
kero zote ambazo umeniambia hapa mbele ya wakuu wa idara na watendaji ofisini
nimezipokea na niko tayari kwa lolote kwani uwezo ninao” alisema Mahiza
Alisema kinachotakiwa ni kufanya
kazi kwa uwazi na uwajibikaji ili kuwaletea maendeleo wananchi na kudai kuwa
yeyote ambaye ataonyesha ukiukwaji wa maadili ni vyema akajiengua mapema.
Mwisho
Mkuu wa Mkoa mpya wa Tanga, Mwantumu Mahiza, akizungumza na wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na viongozi wa vyama vya siasa mara baada ya makabidhiano na mtangulizi wake aliehamishiwa Mkoa wa Katavi.
No comments:
Post a Comment