Nabii aliamini atafufuka na nguvu za kupambana na mapepo, akazikwa akiwa hai.. Kilichofuatia je?
Nimekutana na stori hii kutoka Zimbabwe inamhusu Nabii mmoja kutoka nchi hiyo kufariki akiwa kwenye mishemishe za kupata nguvu za ziada ili akemee mapepo.
Nabii huyo Shamiso Kanyama alifatwa
na familia moja wakamuomba aje nyumbani kwao ili afanye maombezi
kuondoa mapepo yaliyokuwepo kwenye nyumba ya wanafamilia hao.
Nabii huyo akaenda kufanya maombezi na
wanafamilia hao… Wakiwa katika maombezi hayo, nabii huyo alidai kuwa
roho mtakatifu amezugumza nae na kuwaomba wanafamilia hao kuchimba
kaburi nje ya nyumba ili wamzike akiwa hai, alafu akifufuka atakuwa na
nguvu mpya ya kuendelea na maombezi hayo.
Baada ya kuona nabii huyo hatoki kaburini, wanafamilia hao wakaamua
kufukua kaburi ili kumtoa nabii huyo na ndipo walipogundua kuwa tayari
amefariki.Wanafamilia hao wamekamatwa na wameshitakiwa kwa kosa la mauaji.
Kwa habari , matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment