Uchina yakana udukuzi nchini Marekani
Uchina imetaja kama kukosa kuwajibika ipasavyo kwa Marekani kudai kuwa
wadukuzi wa Uchina ndio waliosababisha taarifa za ofisi za
serikali ya Marekani.
Wizara ya mambo ya nje ya Uchina imesema ni
vigumu kujua chanzo cha udukuzi huo na kwamba dhana isiyo na ushahidi
wowote wa kisayansi haitasaidia.Shirika la ujasusi la FBI chini Marekani linachunguza ni kwa namna gani wadukuzi wa komputa waliweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne .
Ofisi ya utumishi ya nchini hiyo inasema karibu watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo.
No comments:
Post a Comment