Kamera za barabarani zikamnasa Mourinho akiwa spidi, Ishu ikafika mahakamani!!
Nchi za wenzetu sheria za barabarani
zimekua zikizingatiwa sana na imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na
ajali zinazoweza kuzuilika mara kwa mara tofauti na hapa kwetu.
Kwa mfano ukipita kwenye taa ambazo hazijakuruhusu hata kama hakuna magari lazima utakamatwa na kuchukuliwa hatua.
Kuna kesi ambayo inamkabili kocha wa Chelsea, Jose Mourinho baada ya mahakama kumfungia kuendesha gari kwa miezi sita baada ya kuendesha kwa kasi katika eneo ambalo haliruhusiwi.
Mourinho alifanya kosa hilo Septemba mwaka jana na kunaswa na kamera akiendesha spidi 60 eneo alilotakiwa kuendesha spidi 50
Katika hukumu iliyotolewa Mahakama ya Staines Magistrates
jana, kocha huyo mwenye miaka 52 ametakiwa pia kulipa faini ya Pauni
910 kwa kuendesha kwa spidi 10 zaidi ya kiwango kinachotakiwa.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment