Mama kakasirishwa mtoto wake kupelekwa kwenye ushirikina na Bibi yake..
Leo inatokea Tabata Dar es
Salaam ambapo mama mmoja analalamika mtoto wake wa miaka saba anafanyiwa
mambo ya ajabu na bibi yake, kuna wakati anamchukua usiku na kumpeleka
mahali ambako wanakutana na kufanya mambo ya kishirikina.
Mtoto huyo amesema bibi yake huwa
anakuja usiku na kumfunga kamba alafu anampeleka sehemu ambapo anakuta
watu wengine wakiwa wamefungwa minyororo… wanapewa damu pamoja na
nyama za watu na baadaye anamrudisha kabla hakujakucha.
Mama wa mtoto huyo anasema alihisi mtoto
wake muda mrefu lakini hakuwa na wasiwasi kwani alikua anaogopa
kumvunjia heshima mama yake mzazi… baada ya kuona tatizo linaendelea
ameona ni bora watu wafahamu ili aweze kupata msaada.
Mama huyo amesema ameenda katika makanisa mbalimbali na anaamini ni Mungu pekee ndiye atakayemuokoa mwanae.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment