Monday, June 8, 2015

MANCHESTER UNITED KLABU YENYE THAMANI ZAIDI DUNIANI

Manchester United ndio klabu yenye thamani kuliko zote duniani.

Manchester-United-v-Queens-Park-Rangers-Premier-League
Klabu ya Manchester United ya nchini England imetangazwa kuwa klabu yenye thamani kuliko zote duniani kufuatia utafiti uliondeshwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita , utafiti uliohusisha klabu kubwa za soka duniani .
Thamani ya United imeongezeka maradufu kutokana na mikataba kadhaa ya udhamini na biashara ambayo imekuwa ikiingia kila mara chini ya uongozi wa Mkurugenzi wa klabu hiyo Ed Woodward .
Chini ya uongozi wake thamani ya United imekuwa kubwa hali ambayo imefanya timu hii kuwa na fedha ambazo zinaipa kiburi cha kuwa na uwezo wa kufanya usajili wa nguvu bila kuhofia minyororo ya kanuni ya financial fair play .
Bayern Munich wanashika nafasi ya pili katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa kuliko zote duniani .
Bayern Munich wanashika nafasi ya pili katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa kuliko zote duniani .
United inafuatiwa na klabu za Bayern Munich na Real Madrid ambazo zimefuatana katika orodha kwenye nafasi ya pili na ya tatu huku Manchester City na Chelsea zikikamilisha orodha ya 5 bora .
Fc Barcelona ambayo ubingwa wa ulaya iliyoutwaa juzi umeiongezea kipato cha paundi milioni 28 iko kwenye nafasi ya sita nyuma ya Man City .
Sababu kubwa ya kupanda kwa thamani ya Manchester United ni Mkurugenzi wake Ed Woodward ambaye chini ya uongozi wake klabu hii imeingia mikataba mingi yenye thamani kubwa .

Orodha kamili ya klabu zenye thamani kubwa kuliko zote duniani.
Nafasi Klabu Thamani (US$m) Nafasi kwa mwaka 2014 Mabadiliko tangu mwaka 2014 (US$m)
1 Manchester United 1206 3 467
2 Bayern Munich 933 1 36
3 Real Madrid 873 2 104
4 Manchester City 800 5 290
5 Chelsea 795 7 293
6 Barcelona 773 4 151
7 Arsenal 703 6 198
8 Liverpool 577 8 108
9 Paris Saint-Germain 541 10 217
10 Tottenham Hotspur 360 12 111
11 Juventus 350 13 103
12 Borussia Dortmund 326 9 -1
13 FC Schalke 04 302 11 -12
14 AC Milan 244 14 8
15 Everton 228 20 107
16 West Ham United 209 24 97
17 AS Monaco 202 New (n/a)
18 Southampton 183 30 86
19 Galatasaray 177 17 36
20 Inter Milan 160 15 7
21 Aston Villa 155 23 40
22 Newcastle 155 27 53
23 Atletico Madrid 151 19 24
24 Napoli 147 21 27
25 Ajax 145 16 -4
26 Stoke City 140 41 65
27 Swansea 135 New (n/a)
28 Bayer Leverkusen 135 22 19
29 Sunderland 134 32 40
30 Crystal Palace 133 New (n/a)
31 Marseille 129 33 38
32 Stuttgart 121 28 19
33 Fenerbahce 120 35 33
34 Celtic 120 38 36
35 Roma 117 26 9
36 Wolfsburg 116 34 25
37 West Brom 115 42 42
38 Lyon 111 25 1
39 Valencia 107 29 8
40 Benfica 103 39 20
41 Hamburg 103 18 -35
42 Leicester City 102 New (n/a)
43 Sao Paulo 95 48 40
44 Werder Bremen 88 31 -6
45 Borrusia Monchengladbach 86 Mpya (n/a)
46 PSV Eindhoven 86 45 27
47 Sevilla 81 40 4
48 Corinthians 79 36 -8
49 Lazio 78 44 16
50 Fiorentina 76 Mpya (n/a)

No comments:

Post a Comment