Watoto kunufaika na dawa mpya za ARV
Watoto
walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa
mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo
zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto
wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la
kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto Duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel
Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa
hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto
kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema
haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa
za kupunguza makali.Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi,
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment