Picha sita za Mastaa wa Real Madrid kwenye jezi zao mpya
Klabu ya Real Madrid
imezindua jezi tayari jezi mpya ambazo watazitumia kwenye msimu ujao wa
soka katika mashindano tofauti kuanzia Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu ya
Hispania na michuano mingine.
Jezi hiyo ambayo imetengenezwa na
kampuni ya ADIDAS ambao ndio wadhamini wa mabingwa hawa mara 10 wa
michuano ya Ulaya, imenakishiwa kwa rangi nyeupe ambayo ni rangi ya
utamaduni ya Real Madrid huku ule weupe ukiwa unang’aa zaidi kuliko ilivyozoeleka kawaida.
Wachezaji wa Real Madrid akiwemo nahodha Iker Cassillas
wameonekana wakiwa wamevalia jezi hii kwa mara ya kwanza wakiionyesha
katika uzinduzi wake na tayari imeshaingia sokoni tayari kuuzwa kwa
mashabiki wa klabu hiyo.
Uwepo wa Iker Cassilas kwenye
matangazo ya jezi hizi umewachanganya wengi kutokana na taarifa
zilizoenea kila mahali kuhusiana na nyota huyo kuwa yuko mbioni kuihama Real baada ya kuitumikia kwa muda mrefu kufuatia mipango ya klabu hiyo ya kumsajili kipa wa Manchester United, David De Gea.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment