Isikie hii ya nyuki kusimamisha safari ya ndege kwa zaidi ya saa mbili..
Mwaka 1996 ndege ya Boeing 757 ilikuwa
imebeba abiria 189 ilipata hitilafu ikiwa ni dakika tano baada ya
kuondoka kufuatia kifaa cha kupima mwendo kasi wa ndege kuzibwa na kiota
cha nyuki hali iliyoleta taharuki kubwa miongoni mwa abiria.
Leo
kuna hii habari ambayo imeingia kwenye headlines inayofanana na hiyo
imetokea huko Uingereza, ambapo abiria walilazimika kukaa kwa masaa
mawili baada ya nyuki kuingia kwenye moja ya mitambo ya injini za ndege
hiyo na kutishia usalama wa abiri waliokua tayari kuondoka.
Ndege hiyo inayoitwa Flybe yenye namba za usajili BE384 iliyokuwa ikitoka Southampton kuelekea Dublin ikiwa na jumla ya abiria huku wahandisi walilazimika kutafuta mbinu ya kumtoa mdudu huyo.
Taarifa kutoka kwa shirika hilo
zilieleza kuwa nyuki huyo alikuwa ndani ya mitambo muhimu ambayo
ingehatarisha maisha ya abiria wake wakiwa angani hivyo iliwalazimu
kumtoa kwanza kwanza kabla ya kuendelea na safari.
No comments:
Post a Comment