Maaskofu wanyanyasaji sasa mashakani
Papa
Francis ameidhinisha kuundwa kwa idara mpya itakayokuwa na mamlaka ya
kuwawajibisha maaskofu wa kanisa katoliki wanaokosa kuwachukulia hatua
wale waliochini ya usimamizi wao na wanaotuhumiwa kuwanyanyasa watoto
kingono .
Mabadiliko hayo yanafanyika baada ya malalamiko mengi kutolewa na waathiriwa wa vitendo hivyo dhalimu.Sheria za dini hiyo, ziitwazo Canon law zilikuwa zimetoa mwongozo wa hatua gani zichukuliwe dhidi ya maaskofu wanaotelekeza wajibu wao lakini uongozi wa Vatican haujawachukulia hatua wale wanaofumbia macho makosa ya unyanyasaji wa kingono unaofanyika katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment