Sokwe ni walevi Hodari :Utafiti
Watafiti ambao wamekuwa wakiwachunguza sokwe nchini Guinea wamegundua kuwa sokwe wamefanya mazoea ya kukwea minazi na kubugia mvinyo
Utatafiti huo wa miaka 17 umebaini kuwa sokwe hao hutumia matagaa kuchovya ndani ya vibuyu vya mnazi na kisha kunywa.
Kwa wakati mmoja sokwe mmoja alichovya sana buyu la nazi ''hadi akalewa''.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la ''the Royal Society Open Science'' ulionesha wazi kuwa chokwe wanapenda sana mnazi.
Katika eneo la Bossou nchini Guinea, wenyeji wengi ni wagema wa pombe ya mnazi.
Watafiti hao walipigwa na butwaa sokwe walitumia sponji kutumbukiza ndani ya vibuyu vya mnazi kisha wakanyonya tembo.
Utafiti uligundua kuwa kila sokwe alikuwa akibugia takriban mililita 85 ya pombe hiyo sawa na chupa moja hivi ya mvinyo.
Asilimia kubwa ya wale waliobugia pombe hiyo walilewa na kisha kulala.
Dakta Kimberley Hockings kutoka chuo kikuu cha Oxford Brookes na kituo maalum cha utafiti wa wanyama cha Ureno alisema mvinyo huo wa nazi una takriban asilimia 3% ya tembo.
Awali ilidhaniwa kuwa tembo inaweza kuwaua wanyama lakini sasa utafiti huu mpya unaibua maswali mengi tu ambayo bila shaka yanahitaji utafiti zaidi haswa miongoni mwa wanyama wengine, alisema dakta Kimberly.
Kwa hivyo ukipata mnazi wako umepungua kwa kiasi kikubwa usiwe mwepesi kuwalaumu binadamu, labda sokwe wamegundua buyu lako umelificha wapi.
No comments:
Post a Comment