Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili na cha sita. Kituo pia kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246
HABARI LEO
Mkaguzi wa Vyakula na Dawa toka Mamlaka ya TFDA, John Mosha
amesema watu wanaotumia dawa mbalimbali kuongeza na kupunguza ukubwa wa
maumbile yao wako katika hatari ya kupata saratani ya ngozi kutokana na
dawa wanazotumia kuaminika kuwa zina viambata vya sumu.
Baadhi ya dawa zilizopigwa marufuku ni pamoja na hip up cream, breast cream, lift up na fem tight.
Mosha amesema dawa hizo zina viambata sumu ambazo vinaingia kwenye ngozi na kusababisha saratani ya ngozi.
HABARI LEO
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe anatakiwa ajiuzulu nafasi yake kutokana na hukumu aliyopewa na Mahakama ya Moshi juzi kumuaibisha.
Mbowe alikutwa ana hatia Mahakamani hapo kwa kesi ya kumpiga Msimamizi wa Uchaguzi mwaka 2010 ambapo Nape amesema Kiongozi huyo hana sifa ya kuwa kiongozi kwa kuwa hana kifua kigumu cha kuzuia hasira.
“Mtu mzima ukiwa umejifunga taulo na
mtoto akaja kuichukua hutakiwi kumkimbiza mtoto, badala yake
unachutama.. ukimbkimbiza na wewe utaonekana akili yako kama mtoto”— Nape Nnauye.
Nape amesema CHADEMA imejijenga kwa misingi ya ubabe na akawataka vijana vijana kuwa macho na kujihadhari.
MTANZANIA
Waziri Dk. Harrison Mwakyembe amekuwa kada wa 37 kuchukua fomu ya kugombea Urais CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.
Dk. Mwakyembe amesononeshwa na mikakati miovu dhidi ya Lowassa wakati alipokuwa akijibu swali kama ana kinyongo na Lowassa.
“Naapa mbele ya MUNGU sina chuki na mtu
yoyote kwa kuwa lile suala (RICHMOND) halikuwa langu bali lilikuwa la
Bunge… Kumtaja MUNGU ni vibaya sana, nikisema uongo atanilaani”—Dk. Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe
amesema huwa anasononeshwa na baadhi ya watu wanaosambaza maneno kuwa
bado ana chuki na Lowassa na alishtushwa kupigiwa simu kwamba anatumia
mitandao ya kijamii kumchafua.
“Niliripoti Polisi na TCRA na nilipata
Ushirikiano uliofanikisha baadhi ya wahusika kukamatwa.. kibaya zaidi
mmoja ya waliokamatwa ni mpambe wa Wanaogombea Urais”—Dk. Mwakyembe.
MTANZANIA
Moses Mongo ambaye ni Mratibu wa Kanda
ya Ziwa kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa (UNA-TANZANIA) amesema
wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaongoza kwa utoaji wa mimba kwa njia za
kienyeji kwa kutumia mwarobaini na bluu ya kuweka kwenye nguo nyeupe.
Mongo alisema katika utafiti walioufanya mwaka 2014 katika Vyuo Vikuu vinne Kanda ya Ziwa wamebaini wanafunzi kutoa mimba kienyeji.
“Utafiti tuliofanya 2014 kwa kuzungumza
na wanafunzi kila Chuo au Shule tumebaini wapo wanafunzi waliotoa mimba
na wapo waliofariki kwa kutoa mimba lakini kwa kificho”—Moses Mongo.
Mongo alisema katika
mazungumzo na wanafunzi hao walieleza kuwa suala la utoaji wa mimba ni
la kawaida na matumizi ya kondomu huwa ni pale wanapoanza uhusiano kabla
ya kuzoeana.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment