Tottenham kumsajili nyota wa Ufaransa .
Klabu ya Tottenham Hotspurs iko mbioni kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa As Monaco Anthony Martial baada ya klabu hizo mbili kuanza mazungumzo huku kukiwa na dalili kubwa za kufikia makubaliano .
Martial ametokea kumvutia kocha wa Spurs Mauricio Pochettino kwa kiwango alichoonyesha msimu huu na amefunga mabao 8 katika michezo zaidi ya 20 ya ligi ya Ufaransa huku akiiongoza Monaco kufika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa .
Martial ana umri wa miaka 19 na hii inamaanisha kuwa bado ana mengi ya kujifunza huku kukiwa na uwezekano wa kuongezeka kwa kiwango na thamani yake katika soko la usajili na Spurs huenda ikapata faida kubwa endapo itaamua kumuuza hapo baadae .
Pamoja na hayo Pochettino huenda akawa anamsajili Martial kama mbadala wa mshambuliaji Harry Kane ambaye tayari ameanza kuwaniwa na baadhi ya klabu kubwa nchini England ikiwemo Manchester United ambao wamekuwa wakihusishwa na usajili wake .
Spurs kwa miaka mingi imekuwa klabu ambayo inauza wachezaji kwa timu kubwa hali ambayo imewafanya wawe tayari kwa kusaka wabadala .
Katika miaka ya hivi karibuni Spurs imewauza Luka Modric , Gareth Bale , Dimitar Berbatov na Michael Carrick huku kiwa tayari kusajili wachezaji wengine kujaza mapengo yao.
No comments:
Post a Comment