Beki mpya Chelsea kawasili, ila usitegemee kumuona Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Klabu ya Chelsea ya Uingereza ilimsajili beki wa kimataifa wa Senegal aliyekuwa anaichezea klabu ya FC Nantes ya Ufaransa Papy Djilobodji kwa dau la pound milioni 3, Chelsea ilimsajili Papy Djilobodji
katika dakika za mwishoni kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hivyo
Septemba 4 ndio siku ambayo amewasili katika uwanja wa mazoezi.
Papy Djilobodji aliwasili katika uwanja wa Cobham ambao ndio unatumiwa na Chelsea kama uwanja wao wa kufanyia mazoezi na kukabidhiwa jezi ya Chelsea. Papy Djilobodji aliyesaini mkataba wa miaka minne ya kuichezea Chelsea, hayupo katika list ya wachezaji watakao cheza hatua ya makundi katika michuano ya UEFA.
Beki huyo atakuwa akivaa jezi namba 15 ila kwa sasa hatutomuona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwani Chelsea haijajumuisha jina lake, hivyo atakuwa akicheza mechi za Ligi Kuu pekee.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment