Mwanamke ashinda kesi kujidunga mayai ya uzazi.
Mwanamke
ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu
wake ameshinda kesi mahakanani na kuruhusiwa kufanya hivyo.
Mwanamke
huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya bintiye
kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa.Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mamake amzalie watoto wake. Lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita.
Hata hiyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu.
Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliawaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.
BBC
No comments:
Post a Comment