Friday, June 24, 2016

UINGEREZA IMEAMUA

Uingereza yaamua kujiondoa kwenye EU

Asilimia kubwa ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya maoni wakiitaka ijiondoe kwenye muungano wa bara Ulaya EU.
Huku asilimia kubwa ya kura zikiwa zimekwisha hesabiwa, asilimia 52% ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya kumaliza uanachama wa Uingereza ndani ya EU uliodumu miaka 43.
Watu wanaoishi katika mji London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Wandani wa maswala ya afisi ya waziri mkuu bwana David Cameron,wanasema kuwa sasa Britain imeingia katika eneo jipya.
Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanahofu athari za kujiondoa kwa Uingereza kwenye muungano huo utabainika katika masoko ya hisa huku kukitarajiwa athari kubwa kiuchumi kisiasa ndani na nje ya bara Ulaya
Sarafu ya Euro imepanda katika masoko ya fedha huku Paundi ya Uingereza ikiendelea kuporomoka ikiwa ni ishara kuwa wafanyabiashara wanatarajia Uingereza kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya.
Kwa mujibu wa ripoti waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa wengi.
Hadi sasa ni majimbo machache ndio hayametangaza matokeo yao na inaonyesha mchuano ni mkali kati ya wanaotaka kubakia na wale wanaotaka Uingereza kujiondoa ndani ya Umoja huo wa Ulaya.
BBC

No comments:

Post a Comment