MAPYA DODOMA
Pichani ni Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia akizungumza jambo mbele ya vyombo vya habari baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge Mapema leo asubuhi mjini Dodoma.
Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni Wakiongozwa na msemaji wa kambi hiyo Mh.James Mbatia wameingia ndani na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge huku wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi na Plasta Wakidai Naibu Spika anakandamiza demokrasia ndani ya Bunge na kwamba wanaendeleza msimamo wao wa kutokuwa na imani na Naibu Spika Dkt . Tulia Ackson MwansasuHii ni wiki ya pili mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwa kile wanachodai kutokuwa na imani nane.
Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi na plasta mara baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na kuzungumza na vyombo vya habari mapema leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment