Maji machafu yakiwa yametuwama hadi
kubadilika rangi na kusababisha mazalia
ya mbu na kuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo la barabara ya 15 Swahili Street.
Ngamiani Kusini Tanga.
Mbali ya jitihada za halmashauri ya jiji kuisafisha inadaiwa kuwa baadhi ya kaya ni chanzo cha mifereji kuziba kwa kutupa takataka na kuiacha kuisafisha.
Wataalamu wa mazingira wameiambia tangakumekuchablog kuwa ni vyema sheria ndogondogo kufuatwa ili kuwezasha mji kuwa msafi na kuchukuliwa hatua kwa wanaokaidi kufanya usafi na kuweka mazingira katika maeneo yao na kuacha dhana ya kuwa Serikali ndio yenye jukumu la kuisafisha.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment