Tuesday, June 28, 2016

HODGSON ATIMKA UINGEREZA

Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu

Saa chache tu baada ya timu ya kandanda ya Uingereza kubanduliwa nje ya mashindano ya mwaka huu ya Euro 2016, Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu wadhfa wake.
Hodgson alikuwa ameshuhudiwa uingereza ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Iceland katika mkumbo wa 16 bora huko ufransa.
Kocha huyo mwenye umri wamiak 68 amekiongoza kikosi hicho cha Uingereza kwa miaka 4 sasa.
Hodgson alichukuwa wadhifa huo kutoka kwa kocha muitaliano Fabio Capello aliyetimuliwa kufuatia matokeo duni.
Hata hivyo kocha huyo hajakuwa na wakati mzuri kileleni mwa Uingereza, Hodgson ameiongoza Uingereza kushinda mechi tatu tu kati ya 11 alizoshiriki katika michuano mikubwa ya dunia .
Lakini kitumbua chake kiliingia mchanga baada ya Iceland - yenye jumla ya watu 330,000 - na moja kati ya timu za mataifa yaliyoorodheshwa ya chini kabisa katika orodha ya FIFA ilipoinyuka Uingereza.
BBC

No comments:

Post a Comment