Donald Trump anusurika kuuawa
Mwanamume mmoja
raia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa kupora bunduki ya afisa mmoja wa
polisi katika mkutano wa kisiasa wa Donald Trump, amewaambia wapelelezi
wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi na kumuuwa mgombea
huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican.
Kwa mjibu wa
stakabadhi za mahakama, Michael Sandford anasema kuwa aliendesha gari
hadi Las Vegas akiwa na nia ya kumpiga risasi Bw Trump siku ya
Jumamosi.Awali Donald Trump alimtimua Maneja wake wa kampeni Corey
Lewandowski kwa kutofautana naye katika kauli zake.Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemlaum Trump kwamba kauli zake ni za hatari
BBC
No comments:
Post a Comment