Saturday, June 25, 2016

WATU 20 WASOMBWA NA MAJI MAREKANI

Mafuriko yawaua watu 20 Marekani

Zaidi ya watu 20 wamefariki kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba jimbo la magharibi la Virginia.
Gavana wa jimbo hilo amesema mafuriko hayo yamesababisha hasara kubwa huku majumba karibu elfu 60 yakikatiziwa umeme.
Imebidi baadhi ya watu kuokolewa ,kutoka mapaa ya majumba walikotorokea mafuriko hayo.
Kinaya ni kuwa upande mwengine wa nchi hiyo hasa katika jimbo la California hali ya kiangazi na joto jingi imesababisha mioto .
Katika eneo hilo watu wawili wamefariki huku wengine mamia wakilazimika kuyahama makaazi yao.
BBC

No comments:

Post a Comment