Ibada ya kumkumbuka
mbunge wa Uingereza aliyepigwa risasi na kuuwawa juma lililopita Jo
Cox, itaandaliwa leo Jumapili katika makanisa mawili huko Birstall -
West Yorkshire.
Kitabu cha maombolezo pia kitafunguliwa kwa wale
ambao wanataka kutoa rambirambi zao kwa mwanasiasa huyo aliyeuwawa siku
ya Alhamisi alipokuwa akienda kwenye kituo cha upasuaji, katika eneo
bunge lake.Hapo jana familia ya mbunge huyo, ilifika mahala aliposhambuliwa na kuzingirwa na watu wa Birstall.
BBC
No comments:
Post a Comment