Wavuvi Kojani waokota bawa la ndege kubwa
Pemba. Wavuvi wa Kisiwa Kidogo cha Kojani Wilaya ya Wete, Pemba, wameokota kipande cha bawa linalodhaniwa ni mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea Machi 8, mwaka 2014.Bawa hilo lenye urefu wa futi nane na inchi moja, limeokotwa majini katika mapango eneo la Ng’ombe nyuma ya Kisiwa cha Kojani.
Wavuvi waliookota bawa hilo, Chungua Hamad Chungua, Juma Mbwana Kombo, Mbwana Bakar Mhunzi, Hamad Chungua Faki na Bakar Hamad Chungua walisema lilikuwa ndani ya mapango na wanahisi huenda lilikuwapo muda mrefu kwani limeanza kuota kutu.
No comments:
Post a Comment