Hatua ya makundi Euro 2016 imemalizika, list ya timu zilizoingia 16 bora
Rasmi usiku wa June 22 2016 hatua ya Makundi ya michuano ya Euro 2016 imemalizika kwa michezo ya Kundi F na D kuchezwa, tumeshuhudia Sweden akikubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Ubelgiji, wakati Ireland ameifunga Italia kwa goli 1-0.
Kwa upande wa Ureno wao wamelazimisha sare ya goli 3-3 dhidi ya Hungary, wakati Iceland walimfunga Austria kwa goli 2-1, michuano hiyo sasa imeingia hatua ya 16 bora na itaanza Jumamosi ya June 25 2016.
No comments:
Post a Comment