Friday, June 17, 2016

KUNGUNI WAVAMIA MATATU (DALADALA ) KENYA

Kunguni wavamia matatu Nairobi

Magari mengi ya usafiri jijini Nairobi, Kenya, maarufu kama "matatu" yana kunguni, kwa mujibu wa gazeti la standard la nchi hiyo.
Kondakta mmoja anaripotiwa kuliambia gazeti la Standard, kuwa wadudu hao wanatishia kuharibu biashara ya kutoka na sababu kuwa watu wengi uhofia kupanda "Matatu"
Wadudu hao husambazwa na wateja kutoka kwa nyumba zao bila kujua, ambao kisha hubaki kwenye viti vya magari.
Sasa wahudumu wa sekta ya usafiri jijini Nairobi, wameanzisha kampeni ya kuangamiza kungunu hao kwa kunyunyiza dawa na pia kuwataka abiria kutoa habari ikiwa wataona wadudu hao.
BBC

No comments:

Post a Comment