Saturday, June 18, 2016

ASASI ISIYO YA KISERIKALI YA EMPOWER YANOGESHA SIKU YA MTOTO WA ARFIKA



Tangakumekuchablog
Tanga, MKUU wa Wilaya ya Mkinga Tanga, Mboni Mgazza, amesema hatomvumilia mzazi yoyote ambaye mtoto wake haendi shule na kusema kuwa msako wa kuwasaka nyumba mmoja mmoja atauanzisha.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika juzi iliyofanyika Kiwilaya kijiji cha Mwanyumba kata ya Bwiti Tarafa ya Maramba Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, alisema wimbi la watoto wasioenda shule linaongezeka.
Alisema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatumikisha watoto wao kwenye kazi za mifugo na kilimo na kusahau umuhimu wa kumpatia elimu ambayo itamsaidia katika maisha yake ya mbeleni.
“Leo tunaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, tumeona changamoto wanazozipata na baadhi yao kunyanyaswa hata na wazazi wao, hili sitoweza kulivumilia katika Wilaya yangu, alisema Mboni na kuongeza
“Ofisi yangu itafanya msako wa nyumba kwa nyumba  kuwafichua wazazi ambao wamewafingia ndani watoto wao na kuwakosesha haki ya msingi ya kupata elimu’alisema
Akizungumzia manyanyaso ya watoto wanaopata kutoka kwa baadhi yawatu ikiwemo kuwafungia ndani iwe kwa  ulemavu au chuki, Mboni alisema kwake hatolivumilia na kuitaka jamii kuwafichua watu wenye tabia hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Empower Sociaty Build The Nation (TBN) ambaye yuko na kituo cha watoto, Devid Poul, aliitaka jamii kuwasaidia watoto wanaolelewa katika vituo vyabkulelea yatima.
Alisema vituo vingi vya watoto vinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mahitaji muhimu ya vykula, nguo na madawa pamoja na miundombinu kwa walemavu.
“Tuko na changamoto nyingi katika vituo vyetu vya kulea watoto  ikiwemo madawa na mahitaji ya kila siku ya binadamu, tunaomba wenye uwezo kuwasaidia ili nao kuweza kuishi kama wenzao.
Alisema misaada ambayo wamekuwa wakipata kutoka kwa baadhi ya watu imekuwa haitoshelezi na kukidhi haja kwa watoto hivyo ni vyema jamii kuwaangalia kwa jicho la pili.
                                                  Mwisho


 Mkurugenzi wa Asasi Isiyo ya Kiserikali ya Empower Sociaty Buld The Nation (ESBN), David Poul (kushoto) akipewa pongezi na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mkinga baada ya kufanikisha msaada wa simu kwa askari Polisi Wilayani humo kukabiliana na uhalifu pamoja na upitishaji wa mali za magendo na Wahamiaji haramu.
Mkurugenzi huyo wa ESBN alitoa msaada huo uliotolewa na Kampuni ya Masawasiliano ya Tigo na kusema kuwa utaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kwa Polisi kwa kufanya mawasiliano ambayo huduma yake itakuwa bure.

 Wanafunzi wa shule ya Mwanyumba Tarafa ya Maramba Wilayani Mkinga Mkoani Tanga wakifurahia zawadi pamoja na mwalimu wao(alievaa miwani) zilizotpolewa na World Vision ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika juzi iliyofanyika Kiwilaya Mwanyumba.

No comments:

Post a Comment