Monday, June 27, 2016

TP MAZEMBE WATUA DAR KWA MBWEMBWE

MAZEMBE WATUA BONGO NA MASHABIKI ZAIDI YA 500

Kuelekea katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kesho Jumanne saa 10:00 jioni, uongozi wa Klabu ya Yanga umesema kuwa wanatarajia kuwapokea zaidi ya mashabiki mia tano wa TP Mazembe ambao watakuwepo uwanjani kuishangilia timu yao.

Licha ya Yanga kutangaza kuwa mchezo huo  utakuwa ni bure ambapo unatarajia kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema tayari wameshapokea taarifa kutoka kwa wapinzani wao hao kuwa watakuwa na mashabiki zaidi ya mia tano kutoka nchini DR Congo kwa ajili ya kuisapoti timu yao.
Mashabiki wa TP Mazembe wanajulikana kwa kuwa na nguvu kubwa ya kushangilia bila kujali wakiwa nyumbani au ugenini, ambapo walipowahi kuja nchini miaka kadhaa iliyopita kucheza dhidi ya Simba walikuwa na kikundi cha ngoma kilichokuwa kivutio kwa mashabiki wengi nchini.  

No comments:

Post a Comment