Watengeneza Pizza watakiwa kusoma zaidi Italia
Kundi la maseneta
wa Italia wametoa wito kwa watengenezaji wa Pizza kupasi mitihani yao
ili kuboresha viwango vya uundaji wa mlo huo.
Wabunge ishirini na
wawili katika bunge la juu waliwasilisha mswada, ambao ukiidhinishwa
kuwa sheria,itapendekeza kusajiliwa kwa taaluma maalum ya
pizzaoli-wapishi wa pizza.Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la habari la Rai,Taaluma hiyo itajumuisha kozi zitakazosomewa kwa jumla ya saa mia moja ishirini itakayo muezesha mwanafunzi kufuzu kwa Diploma.
Katika mapendekezo hayo , wale wanaopania kuwa Pizzaoli wanastahili kupasi mitihani wa kinadharia na wa kivitendo baada ya kusomea sayansi ya chakula,usafi na lugha za kigeni msisitizo zaidi ukipewa lugha ya kiingereza.
BBC
No comments:
Post a Comment