Thursday, June 23, 2016

MAPENZI YA BABA KWA MTOTO

Baba ajiweka tatoo afanane na mwanawe aliyefanyiwa upasuaji

Mzazi  nchini Marekani amenyoa kichwa chake na kuweka mchoro wa tatoo unaofanana na kovu la kichwa cha mwanawe aliyefanyiwa upasuaji.
Josh Marshall,ambaye anatoka Kansas aliingia katika shindano la kila mwaka linaloendeshwa na shirika la hisani kuhusu saratani ya watoto na kushinda taji la #BestbaldDad{baba mwenye kipara kizuri} wikendi iliopita.

Mwanawe alipatikana na uvimbe katika ubongo mnamo mwezi Machi.
BBC

No comments:

Post a Comment