Thursday, June 30, 2016

GAZETI AUSTRALIA LABASHIRI MSHINDI WA UCHAGUZI

Mamba anayebashiri matokeo ya uchaguzi Australia

Gazeti moja nchini Australia limedai kwamba kuna mamba anayeweza kubashiri matokeo ya uchaguzi nchini Australia.
Gazeti hilo la Northern Territory News ni maarufu kwa habari zake katika ukurasa wake wa kwanza.
Huku raia wakisubiri uchaguzi wa siku ya Jumamosi ,gazeti hilo liliweka picha za wagombea wawili wakuu wa uchaguzi huo katika ndoana ya samaki na kumrushia mamba anayeitwa Burt mwenye urefu wa mita 5.1.
Burt alionekana kuifuata picha ya kiongozi wa upinzani Bill Shorten ,lakini baada ya mda akaamua kuitia mdomoni ndoana ya picha ya waziri mkuu Malcolm Turnbull,ikiwa ishara inayoonyesha kwamba ataibuka mshindi katika uchaguzi huo.
''Wanaobashiri tayari wamesema kuwa waziri huyo ataibuka mshindi'', alisema muhariri wa gazeti hilo Matt Williams.
Ubongo wa mamba huyo ni mdogo sana lakini ni miongoni mwa wanyama werevu sana.
Mamba huyo huishi katika mbuga ya wanyama pori ya Crocosaurus Cove na alishiriki katika katika filamu ya Australia Crocodile.
Ni mnyama wa hivi karibuni aliyebainika kuwa mwerevu huku yule maarufu akiwa Pweza Paul,ambaye alifanikiwa kubashiri matokeo ya mechi saba katika kombe la dunia la mwaka 2010 nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment