Mfanyabiashara wa Vinyago soko la
Uzunguni Tanga, Habib Abubakary, akionyesha bidhaa zake kwa wateja waliofika
katika banda lake na kusema kuwa
biashara hiyo inategemea msimu wa watalii na kuitaka Serikali kuwatafutia soko
la ndani na nje ya nchi ili kubiresha kazi zao za mikono.
Wajasiriamali wengi wa kazi za mikono Wanaume na Wanawake wamekuwa wakishindwa kuendeleza ujuzi wao baada ya kazi zao kutokuwa na soko la uhakika.
Hata hivyo baadhi ya wadau waliozungumza na tangakumekuchablog wamedai kuwa wajasiriamali wengi nchini wamelaghafilika na kusahau kuwa kuna soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Wamedai kuwa ndani ya Jumuiya hiyo Wajasiriamali wa Kenya na Uganda wamekuwa wakilitumilia vyema soko hilo na kuweza kuzinadi kazi zao na kupata soko kubwa.
No comments:
Post a Comment