Inawezekana msimu ujao tusimuone Yaya Toure Man City
Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Man City ya England, anaripotiwa kuwa na mipango ya kutaka kuihama Man City na kujiunga na Inter Milan ya Italia.
Toure ana uwezekano wa asilimia 50 za kuondoka au kutokuondoka Man City, hiyo inatokana na kutojua hatma yake ndani ya kikosi cha Man City baada ya kocha wake wa zamani wa FC Barcelona Pep Guardiola kujiunga na kikosi hicho, Toure amebakiza mkataba wa mwaka mmoja Etihad.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Pep Gurdiola alimuuza Yaya Toure mwaka 2010 kuto FC Barcelona kwenda Man City kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 23, hivyo huenda akaondoka kwenda Inter Milan kutokana na kuaminika kuwa huenda akakosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha Guardiola.
No comments:
Post a Comment