Fisi amng'ata mtoto Afrika Kusini
Maafisa wa mbuga ya
wanyamapori Afrika Kusini wamewashauri waweni kuwa makini, baada
ya fisi kumshambulia mtoto wa umri wa miaka 15 alipokuwa amelala ndani
ya hema katika mbuga ya Kruger.
Msemaji wa mbuga za wanyamapori
William Mabasa, aliwashauri wageni kuchukue tahadhari kila wakati, kwa
kuwa kuna wanyamapori wanaowazunguka, na kuwataka wahakikishe kuwa hema
zao zimefungwa vizuri.Mtoto huo alifanyiwa upasuaji ili kupata matibu kwenye mdomo, kutokana na majeraha aliyoyapata kufuatia shambulizi hilo.
BBC
No comments:
Post a Comment