Saturday, June 25, 2016

UGONJWA WA AJABU WAUA WATU 7 WAGONJWA 32

Taarifa iliyotolewa leo kuhusu mlipuko wa ugonjwa usiofahamika Dodoma

June 19 2016, Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia na watoto ilitoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa usiofahamika katika wilaya za Chemba na Kondoa, mkoani Dodoma ambapo wakati huo kulikuwa na jumla ya wagonjwa 21 na vifo 7.
Leo June 25 2016 Waziri Ummy Mwalimu ametoa taarifa kwamba idadi ya wagonjwa imefikia 32 na idadi ya vifo imebakia 7 hii ni baada ya kuongezeka kwa wagonjwa 11 katika kipindi cha wiki moja.
Waziri Mwalimu amesema Wizara ifanya jitihda mbalimbali za kutambua kiini cha ugonjwa huo baada ya kupeleka jopo la wataalamu ili kufanya uchunguzi wa kina pia ameeleza kuhusu sampuli zilizofanyiwa utafiti…….
>>>’Sampuli mbalimbali zikiwemo, haja ndogo, haja kubwa, vinyama vya ini na sampuli za vyakula zilipelekwa katika maabara za mkemia mkuu wa serikali, maabara ya mamlaka ya chakula na dawa ‘TFDA’
>>>’Hadi sasa sampuli za nafaka pekee, zilizofanyiwa uchunguzi katika maabara ya TFDA ndio zilizoonyesha kuwepo kwa uchafuzi wa sumukavu ‘Aflatoxin’ katika sampuli za nafaka hizo’:- Waziri Mwalimu
Waziri ameongeza pia kuna uwezekano mkubwa kwamba ugonjwa huo umesababishwa na ulaji wa chakula kilichokuwa na sumukuvu na kuleta madhara.

No comments:

Post a Comment