Tuesday, June 21, 2016

PICHA 14 MAPANGO YA KITALII YA AMBONI TANGA

 Mkurugenzi wa tangakumekuchablog akivinjari ndani na nje ya Mapango ya Kitalii ya Amboni ambayo ni zaidi ya kilometa 5 ya Mapango ya Mleni ambapo majambazi kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Tanga wamekuwa wakijificha na kufanya uhalifu ukiwemo wa uporaji katika maduka makubwa na vituo vya mafuta (Petrol Station).
Ni hivi karibuni hali ya Sintofahamu ilijitokeza ambapo watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walifanya tukio la mauaji ya watu 8 kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni kisha kutokomea kusikojulikana na taarifa za Kipolisi baadhi ya washukiwa wametiwa mbaroni huku Operesheni ya kuwasaka ikiendelea.



 Lango kuu la kuingilia ndani ya mapango ambapo ndani ni Kiza mithili ya usiku TORORO na nilazima muongozaji kuwa na Tochi ya mwanga mkubwa na ndani kujionea vivutio vya ajabu ambavyo huwezi kuamini.
Ndani ya Mapango hayo kuna uchochoro mwembamba uliopinda na upitapo ni lazima utembee kwa Tumbotumbo na endapo ukikwama itakuwa balaa.(Ila haijawahi kutokea, ni maajabu)
Baadhi ya wageni kutoka Holland waliozungumza na Tangakumekuchablog wamesema vivutio vilivyopo ndani ya Pango hilo hakuna Barani Afrika na kushangaa havitangazwi ipasavyo.
Alisema vivutio hivyo endapo vitatangazwa ndani na nje ya nchi Serikali inaweza kuingiza pesa nyingi na uchumi wa wananchi na Taifa kukuwa.






 Uchochoro ndani Pango ni ajabu. Inasemekana ndani ya Pango hilo kuna njia ambayo inatokea Mkoa wa Kilimanjaro kwa upande mmoja na mwengine unatokea Mombasa nchini Kenya.

Hili ni moja ya Pango ambalo ukichungulia utaogopa kwani huoni mwisho hata ukitupa jiwe utalisikia baada ya dakika kadhaa tena likiwa halijafika mwisho na linakuwa linagonga pembe za Pango. Waongiozaji wanashauri Pango hilo kwa Mtalii wa ndani na nje kutolisogelea kwani lina nguvu mithili ya Sumaku.

No comments:

Post a Comment